Kituo cha faharasi na mpangilio wa taarifa: kimeanza kutengeneza ramani na kuiweka kwenye faharasi ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na mpangilio wa taarifa chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kuandika ramani ya Iraq na kuiweka kwenye faharasi ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya (www.lccis.net) chini ya utaratibu wa kisasa unaotumika duniani (MARC21) na njia ya (RDA) hatua hii ni ya kwanza kufanywa.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Hasanaini Mussawi, amesema “Kituo chetu kinaenda na maendeleo ya dunia katika sekta hii, kila baada ya muda huwa tunaongeza taarifa mpya kwenye faharasi, taarifa itakayo ongezwa kwa sasa ni ramani ya Iraq itakayo kuwa na vitu vifuatavyo: (hali ya hewa, idadi ya wakazi, maeneo ya kawaida, maeneo ya kilimo, maeneo ya ukame, maeneo ya utalii, maeneo ya shuguli za kibinaadamu, vituo vya umeme na maji pamoja na barabara na mawasiliano) kwa vipindi tofauti, hii ni hatua ya kwanza, tunatarajia kuwa na hatua zingine zitakazo angazia nchi za kiarabu na nchi zingine duniani”.

Akabainisha kuwa: “Kazi ya kuandika ramani inahusisha vitu vingi kwa ajili ya kukusanya taarifa na picha kisha kuzipangilia kwa kufuata njia ya kisasa (RDA) chini ya mfumo wa MARC21”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: