Kumaliza uvunaji wa ngano katika shamba la Saaqi

Maoni katika picha
Idara ya shamba la Saaqi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imemaliza uvunaji wa ngano ulio dumu kwa muda wa siku tatu, ambapo wamevuna jumla ya dunam (840), zilizopo katika vitalu tisha, kazi ya kupeleka ngano kwenye kituo cha Ghamaas na Abi Gharq vilivyo chini ya wizara ya kilimo bado inaendelea.

Kiongozi wa mradi huo Ustadh Zaki Swahibu amesema kuwa: “Ngano imevunwa aina mbili, kwanza ni (Bagdad) kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam (360), na aina ya pili ni mbegu ya (Buhuthu/22), kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam (480)”.

Akasisitiza kuwa: “Kufanikiwa kuvuna ngano hii katika jangwa hili lililokuwa halimei kitu, kumetokana na juhudu ya watendaji pamoja na utaalamu wao wa kuanzisha kilimo katika majangwa kama haya, uzowefu uliopatikana katika shamba hili unatarajiwa kuhamishiwa maeneo mengine pia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu”.

Akaendelea kusema: “Pamoja na hivyo bidhaa za shirika la Khairul-Juud na mbolea zao zinamchango mkubwa katika mafanikio haya”.

Kumbuka kuwa shamba la Saaqi lina ukubwa wa dunam (840) zilizopo katika vituo (9) vya umwagiliaji, sita vikimwagilia eneo lenye ukubwa wa dunam (480) ikiwa ni dunam (80) kwa kila ushoroba, vituo vitatu vimeongezwa kwenye mradi wakati wa utekelezaji wa mradi, ambazo zinamwagilia eneo lenye ukubwa wa dunam (360) kila ushoroba ukiwa na dunam (120), maji ya visima ndio yanayo tumika kumwagilia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: