Tunaendelea.. kunapambana pamoja dhidi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
(Tupo pamoja dhidi ya virusi vya Korona) ni kauli mbiu inayo tumiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, iliyo anza tangu mwanzo wa kupatikana kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Kikosi kazi cha kujikinga na maambukizi kilicho undwa na Atabatu Abbasiyya bado kinaendelea kupuliza dawa kwenye majengo na maeneo yote yaliyo chini ya Ataba tukufu pamoja na mji mkongwe na sehemu ya katikati na haram mbili tukufu, aidha wanashiriki katika shughuli ya kupuliza dawa barabara zote za Karbala pamoja na maeneo ya wazi.

Kuhusu upande wa utowaji wa elimu, kitengo cha habari kimechapisha na kugawa maelfu ya vipeperushi sambamba na kuandaa vipindi maalum ambavyo vinarushwa kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel na vituo vya luninga, pamoja na shughuli zingine za kujikinga na maambukizi ya Korona ambayo yamepiga kengele ya hatari hapa Iraq.

Kumbuka kuwa hatua zinazo chukuliwa zimetokana na agizo la Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata maelekezo ya idara ya afya, pamoja na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona hapa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: