Nimefuzu! Kwa jina la Mola wa Alkaaba

Maoni katika picha
Dunia imepambwa rangi nyeusi na imejaa huzuni na majonzi kutokana na kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), katika siku kama ya leo, mwezi ishirini na moja Ramadhani mwaka wa 40 hijiriyya umma wa kiislamu ulipata msiba mkubwa, ulio tikisa arshi ya Mwenyezi Mungu na kuombolezwa na malaika wa mbinguni, Jibrilu akasema: “Wallahi nguzo ya uongofu imevunjika, na nyota za mbinguni zimezimika na bendera ya uchamungu, ameuwawa mtoto wa ammi wa Mtume, ameuwawa wasii wa mtukufu, ameuwawa Ali mridhiwa, ameuwawa bwana wa mawasii, ameuliwa na mtu muovu zaidi ya waovu).

Kiongozi wa waumini (a.s) aliuwawa katika mji wa Kufa usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani mwaka wa arubaini hijiriyya kutokana na jeraha la upanga aliopigwa na Ibun Muljim (laana ya Allah iwe juu yako) akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.

Shekh Mufidi katika kitabu cha Irshaadi ameandika kuwa: (Kiongozi wa waumini –a.s- aliuwawa karibu na wakati wa Alfajiri usiku wa Ijumaa mwezi ishirini na moja Ramadhani mwaka wa arubaini hijiriyya kutokana na jeraha la upanga aliopigwa na Ibun Muljim Almuradi –laana ya Allah iwe juu yake- ndani ya msikiti wa Kufa, watoto wake Hassan na Hussein ndio walio simamia shuguli ya kumuosha na wakaenda kumzika Najafu chini ya usia wake na wakaficha kaburi lake, kutoka na uadui wa bani Ummayya dhidi yake, sambamba na njama mbaya walizokuwa wakipanga kumfanyia…).

Alaamah ibun Twausi ameandika katika kitabu cha Furhatul-Ghuri kutokana na riwaya iliyo pokewa na Habani bun Ali kutoka kwa Mtumishi wa Ali bun Abu Twalib anasema: (Kiongozi wa waumini alipo karibia kufa, alimuambia Hassan na Hussein kuwa, kama nikifa mnibebe nikiwa juu ya kitanda na mnitowe hapa, mnipeleke upande wa Ghariyyiin, mtaona jiwe leupe, fukueni chini ya jiwe hilo mtakuta kaburi mnizike hapo. Akasema: alipo fariki tulimbeba hadi tukafika Ghariyyiin, tukaona jiwe leupe linatoa nuru, tukafukua chini ya jiwe hilo tukakuta kaburi limeandikwa (limeandaliwa na Nuhu kwa ajili ya Ali bun Abu Twalib). Tukamzika katika kaburi hilo na tukaondoka tukiwa na furaha kutokana na namna Mwenyezi Mungu alivyo mkirimu kiongozi wa waumini (a.s).

Mwenyezi Mungu ameitukuza ardhi ya Najafu kwa kuhifadhi miili ya Mitume na mawasii pamoja na waja wema, kama vile Adam, Nuhu, Huud na Swaaleh (a.s). kutoka kwa Fadhili bun Omari Ja’fiy anasema: (Niliingia kwa Abu Abdillahi (a.s) nikamuambia: ninaham ya kwenda Ghura. Akasema: (Kwa nini unaham ya kwenda huko?) nikamuambia: Napenda kumzuru kiongozi wa waumini (a.s). akasema: (Unajua utukufu wa kumzuru?) nikasema: sijui, ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, nijulishe, akasema: (Ukimzuru kiongozi wa waumini tambua kuwa umeizuru mifupa ya Adam na muili wa Nuhu na Ali bun Abu Twalib –a.s-).

Katika kitabu cha Tahdhiib cha Shekh Tusi imeandikwa kuwa Imamu Ali (a.s) alimuusia mwanae Imamu Hassan Almujtaba (a.s): (…Nikifa nizikeni sehemu hii, karibu na kaburi la ndugu yangu Huud na Swaaleh).

Mwenyei Mungu ni mkubwa kwa msiba huu wenye majonzi makubwa katika uislamu, na huzuni kubwa katika nyoyo za waislamu, hakika wanaadamu wamepata hasara kubwa kwa msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: