Idara ya uhusiano na vyo vikuu imetangaza shindano la kijana wa Alkafeel

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano la kijana wa Alkafeel katika mwezi wa Ramadhani, litakalo husisha wanafunzi wa vyuo na shule za Iraq.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Maahir Khalidi amesema kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Shindano litaanza siku ya mwezi (20 Ramadhani) na litaendelea hadi mwezi (28), unaweza kushiriki kwa kupitia telegram au link hii: t.me/alkafeel019”.

Akasema: “Mshirika anatakiwa kujaza fomu maalum halafu ajibu maswali, kutakuwa na washindi (10) watakao patikana baada ya kuwapigia kura wale watakao jibu sahihi”.

Akabainisha kuwa: “Majina ya washindi yatatangazwa katika usiku wa Idul-Fitri, zimeandaliwa zawadi maalumu za washindi pamoja na washiriki wengine”.

Ukiwa na tatizo lolote tuandikie kupitia ukurasa maalum wa mradi wa kijana wa Alkafeel: https://www.facebook.com/AlKafeel.Youths/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: