Tambua yaliyo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kupambana na janga la Korona

Maoni katika picha
Tangu siku za kwanza kutangazwa janga la maradhi ya Korona Atabatu Abbasiyya tukufu imekuwa mstari wa mbele kupambana dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona hapa Iraq, imefanya shughuli mbalimbali za kulinda jamii dhidi ya virusi hivyo, sambamba na kujenga vituo vya afya ndani ya muda mfupi, na kutoa misaada mbalimbali ya kibinaadamu.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Kutokana na kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya kuhusu kulinda afya za wanajamii, Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo na vituo vyake tofauti tangu siku kwa kwanza kupatikana maambukizi ya virusi vya Korona, imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo hapa nchini, imechukua hatua za kiafya na kibinaadamu sambamba na hatua za utowaji wa elimu kwenye vyuo vikuu na shule”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo muhimu yanayofanywa na Atabatu Abbasiyya ni:

  • 1- Shirika la Khairul-Juud limeongeza uzalishaji wa barakoa ili kukidhi soko la ndani na kuziuza kwa bei nafuu.
  • 2- Kupuliza dawa katika mji wa Karbala na mitaa yake.
  • 3- Kuchapisha na kusambaza vipeperushi vya kutoa elimu kuhusu namna na kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na kutengeneza mabango na kuyaweka barabarani.
  • 4- Kuendesha opresheni ya Takaaful, kwa kuzigawia chakula familia za watu wenye kipato kidogo walio athiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
  • 5- Kujenga kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) chenye vyumba vya wagonjwa sitini ndani ya muda usiozidi siku kumi na tano.
  • 6- Kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali kuu ya Hindiyya kusini mwa Karbala, chenye vyumba vya wagonjwa thelathini na tano ndani ya muda usiozidi siku (24).
  • 7- Kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Najafu, chenye vyumba vya wagonjwa (24) kwa kushirikiana na hospitali ya Amirulmu-Uminina (a.s) ndani ya muda wa siku (18) tu.
  • 8- Kutengeneza barakoa na mavazi maalum ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kugawa bure.
  • 9- Kutengeneza vifaa vya kukinga uso kutokana na maambukizi ya virusi vya Korona na kuvigawa katika sekta maalum.
  • 10- Kutengeneza vifaa vya kupuliza dawa na kuviweka katika baadhi ya vituo vya umma na hospitali za Karbala.
  • 11- Kugawa chakula kwa askari wanao simamia marufuku ya kutembea na wale ambao wapo katika vituo vya kazi.
  • 12- Kusaidia kikosi cha madaktari katika kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.
  • 13- Kupuliza dawa kwenye mikoa tofauti.
  • 14- Kuchapisha maelezo ya kiafya na kuweka kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii ikiwa ni program inayo simamiwa na chuo kikuu cha Al-Ameed, Alkafeel pamoja na kituo cha utamaduni wa familia.
  • 15- Kuendesha program mbalimbali za kutoa elimu kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
  • 16- Kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa hauza, vyuo na shule mbalimbali kwa kutumia njia ya mtandao”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo na vituo vyake mbalimbali, inaendelea kupambana na janga hili kwa njia mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: