Vyombo vya habari vimeandaa masafa maalum ya kurusha vipindi vya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa vyombo vya habari vimeandaa masafa maalum ya kurusha vipindi vya mwezi wa Ramadhani vya kila siku, vikiwemo vipindi vya usomaji wa Quráni na kipindi cha Maaidatu-Thaqalaini.

Kiongozi wa kituo cha habari katika Maahadi Ustadh Mustafa Da’miy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kila mwaka huwa tunaandaa vipindi vya kurushwa kwenye vituo vya luninga, ambapo huwa kuna matangazo ya kila siku ya mubashara au yaliyo rekodiwa, vipindi hivyo hurusha usomaji wa Quráni katika michana na nyusiku za mwezi huu mtukufu, vipindi hivyo hutengenezwa kwa ufundi na umaridadi mkubwa katika kituo cha uzalishaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari cha Ataba tukufu, kilicho andaa masafa ya bure inayo rusha picha zenye ubora wa hali ya juu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa vituo vinavyo rusha vipindi hivyo ni (kituo cha Quráni tukufu, Furaat, Aqiilah, Al-Ayaami, Al-Auhad, Alhujjah, Almahdi, Al-Ibaa, Ashaáir, Almimbar, Albayyinaat, Almawaakibu), kituo cha uzalishaji Alkafeel kimechukua jukumu la kutengeneza vipindi na kuvirusha katika luninga zote zinazo onyesha mubashara, wanarusha vikao vya usomaji wa Quráni tukufu katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani kuanzia saa kumi na moja jioni, pamoja na kipindi cha Maaidatu-Thaqalaini”.

Kumbuka kuwa masafa ya bule iliyo tengenezwa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kurusha harakati za mwezi mtukufu wa Ramadhani yanapatikana kupitia anuani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat7A at 7.0 East(W3A)
DOWNLINK:12680.200 H
MOD:DVBS2
QPSK
FEC:5/6
Sr :3250
HD/MPEG-4
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: