Kukamilika hatua ya kumi na nne ya ugawaji wa chakula unaofanywa na wawakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mkoa wa Swalahu Dini

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mkoa wa Swalahu Dini wamemaliza hatua ya kumi na nne ya ugawaji wa chakula kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, pamoja na familia za mashahidi na mayatima kupitia opresheni ya Marjaiyyatu-Takaaful iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa kikosi, akaongeza kuwa: “Ugawaji huu umefanywa sambamba na kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa waumini (a.s), tumegawa jumla ya vifurushi vya chakula (110), vifurushi (60) vya chakula kikavu na (50) vya nyama na mboga za majani, wamepewa mayatima na familia za mashahidi kwa kufuata utaratibu uliopangwa na taasisi ya Ainu katika wilaya ya Dujail”.

Akafafanua kuwa: “Ugawaji huu wa chakula ni muendelezo wa ugawaji mwingi uliofanywa chini ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, kupitia opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kusaidia mafakiri na watu wenye kipato kidogo, sambamba na kufuata muongozo wa mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s)”. akasema: “Tumegawa chakula katika mji wa Dujail, katika mtaa wa Wahdah, Zaharaa (a.s), Answaar, Askariy na kitongoji cha Jumuiyyah”. Akasema kuwa kuna ugawaji mwingine utafanywa siku zijazo.

Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu alihimiza watu wote waonganishe nguvu katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndio Atabatu Abbasiyya ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: