Miongoni mwa shughuli zake za kuhudumia sekta ya elimu imetengeneza (kituo cha vitabu vya masomo) ambayo imekusanya vitabu vyote kwa njia ya mtandao (SDI) unaotumiwa na chuo kikuu cha Al-Ameed.
Mkuu wa maktaba kuu Ustadh Wasim Twaalib Mahdi amesema kuwa: “Program hii ni nzuri kwa wanafunzi wa chuo chetu cha udaktari na vingine, maktaba ya chuo cha Al-Ameed inamakubaliano maalum na wadau wa program hii, inatumika mfumo wa (research for life) katika kutafuta faili, pamoja na mfumo wa (Hinary) chini ya makubaliano hayo, kila kitu kilichopo katika program hiyo kinapatikana kupitia (open aceess)".
Akaongeza kuwa: “Huduma hii imewarahisishia watafiti, wanafunzi, wakufunzi na wengineo, sambamba na huduma ya maktaba ya mtandaoni inayo tolewa na chuo na kupewa kipaombele zaidi wakati huu kwa kutumia mfumo wa (SDI) kutokana na janga la virusi vya Korona”.