Hospitali ya rufaa Alkafeel inamiliki kifaa tiba cha kisasa cha kutibu maradhi ya ubongo kwa wagonjwa wenye umri tofauti na wala hakihitaji matibabu ya upandikizaji wa ubongo kwa mgonjwa.
Daktari bingwa wa upasuwaji wa kichwa Dokta Husaam Ambaar amesema kuwa: Hiki ni kifaatiba cha kisasa kinacho tumika katika matibabu ya ubongo, kwa kutumia kifaa hiki hufunguliwa njia ndogo kwa ajili ya kuingiza kifaa kwenye ubongo na kutibu tatizo lililopo bila kuhitaji upasuwaji mkubwa.
Akaongeza kuwa: Kifaa tiba hiki kinaweza kutumiwa na watu wenye umri tofauti, kiwango ambacho hutobolewa kwenye kichwa kinakuwa ni kati ya (sm 2 – 3), nacho ni kiwango kidogo sana ambacho huwezesha kuangalia ndani ya fuvu la kichwa na kutibu tatizo lililopo bila kusababisha madhara mengine.
Kumbuka kuwa chumba cha upasuwaji wa kichwa katika hospotali ya rufaa Alkafeel kina fivaatiba vingi vya kisasa na vyenye ubora mkubwa kikiwemo hiki cha kutibu ubongo.