Kikosi cha Abbasi kimeandaa vifurushi (3500) vya chakula kwa ajili ya kugawa mikoani

Maoni katika picha
Kikosi kazi kilicho undwa na viongozi wa kikosi cha Abbasi –a.s- cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimeandaa vifurushi (3500) vya chakula kitakacho pewa familia za watu wenye kipato kidogo kupitia mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful na maelekezo ya viongozi wa kikosi.

Kiongozi wa kikosi hicho Sayyid Muhammad Aáraji amema kuwa: “Vifurushi hivyo vina aina mbalimbali za vyakula vinavyo hitajiwa na familia, vitasambazwa kwa wawakilishi wa kikosi waliopo mikoani na wao watafikisha kwa walengwa, kama walivyo omba katika ataba au kwa muwakilishi wa Marjaa Dini kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.

Akabainisha kuwa: “Misaada hii itasaidia kukidhi haja za familia hizo japo kidogo katika mazingira ya marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tunamuomba Mwenyezi Mungu aondoe hili giza katika huu umma”.

Kumbuka kuwa opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, aliye himiza kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: