Kituo cha kuegesha magari Alkafeel baina ya upekee wa kihandisi na utendaji wa kisasa

Maoni katika picha
Mradi wa kituo cha kuegesha magari Alkafeel ni miongoni mwa miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya, sambamba na maendeleo yanayo shuhudiwa ambayo yanapelekea kuwa na kituo kama hiki, kituo hiki ni mfano mzuri na kina uwezo mkubwa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Dhwiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa: “Kituo hiki kinapokea idadi kubwa ya gari za Atabatu Abbasiyya pamoja na kuyafanyia matengenezo, kituo kina sehemu tano tofauti, aidha kina mafundi gereji na madereva mahiri, kituo hicho kilijengwa kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa gari za Ataba, kwani kinakusanya sehemu moja gari zote za Ataba, aidha gari zote zinaweka mafuta (petrol na dissel) sehemu moja, jambo ambalo linasaidia kuokoa muda”.

Akaongeza kuwa: “Kituo cha maegesho ya gari kimejengwa kisasa kwa kutumia vifaa vyenye ubora wa hali ya juu, vyenye uwezo wa kuvumilia mazingira ya joto na baridi, aidha kumefungwa mitambo ya kisasa ya kuzuwia moto”.

Akafafanua kuwa: “Kituo hicho kina sehemu tano. Sehemu ya kwanza ni sehemu za ofisi zenye jukumu la kuandika taarifa za gari yeyote inayo ingia kwenye kituo hicho. Sehemu ya pili ni pampu za kisasa za kuweka mafuta kwenye gari (dissel na petrol) yenye uwezo wa kubeba lita (1,000,000) za mafuta. Sehemu ya tatu ni kwa ajili ya matengenezo madogo madogo ya gari. Sehemu ya nne imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutengeneza gari zilizo haribika kubwa na ndogo na ina vifaa vya kisasa”.

Akaendelea kusema: “Sehemu ya tano imeandaliwa maalum kwa ajili ya kuegesha gari kubwa na ndogo, sehemu hiyo ina ghorofa mbili kubwa, kila aina ya gari imetengewa sehemu yake, kuna sehemu ya gari kubwa, za saizi ya kati na ndogo, ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa gari hizo, gari kubwa zinaegeshwa tabaka la chini na tabaka la juu zinaegeshwa gari ndogo, eneo lote la maegesho linaweza kuingia gari (500) takriban za aina zote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: