Idara ya afya ya Karbala na idara ya mji wa Imamu Hussein wa kitabibu zinaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha pili

Maoni katika picha
Ugeni kutoka idara ya afya ya Karbala na mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu umetembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu pamoja na makamo wake na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo, kwa ajili ya kutoa shukrani ya kukamilika ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu hapa Karbala kinacho itwa (Jengo la Alhayaat la pili) lililojengwa na Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha usimamizi wa kihandisi.

Ugeni huo umeongozwa na mkuu wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala Dokta Swabaahu Mussawi, ambaye ametoa shukrani kwa kukamilika ujenzi huo ulio fanywa kwa muda usiozidi siku 15 na kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu.

Ugeni huo ukasikiliza ujumbe elekezi kutoka kwa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu, aliye pongeza utendaji wao katika kipindi hiki kigumu, wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kuwapa zawadi za kuonyesha kutambua na kujali utendaji wao.

Kumbuka kuwa kazi hii (ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha pili) kilicho tolewa zawadi na hospitali ya rufaa Alkafeel, ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuilinda jamii na maambukizi ya virusi vya Korona, na muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, aliye agiza ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu katika mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: