Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kimeratibu semina ya watumishi wa maktaba katika chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daaru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu semina kuhusu mifumo ya faharasi ya kisasa kwa watumishi wa maktaba katika chuo kikuu cha Imamu Alkaadhim (a.s) kupitia intanet, program ya (ZOOM) itakayo fanyika kwa muda wa saa mbili kwa siku, mada zitahusu mfumo wa (MARC21 na RDA) utajaji wa vitabu na nafasi yake, pamoja na namna ya kupakua na kutumia program ya (KOHA) kwa ajili ya maktaba, ambayo ni miongoni mwa program za kisasa inayo tumiwa na maktaba za kimataifa duniani ikiwemo maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Yamesemwa hayo kwenye mtandao wa Alkafeel na mkuu wa kituo ustadh Hasanaini Mussawi: “Hii ni moja ya semina zinazo andaliwa na kituo kwa ajili ya watumishi wa maktaba za serikali na binafsi, ukizingatia kuwa kituo kina wataalamu wenye uzowefu mkubwa na mbinu za kisasa, mkufunzi wa semina hiyo alikuwa ni Ustadh Bahaau Twalibu ambaye ni kiongozi wa idara ya msaada wa kitalamu, na Ustadh Ahmad Muhammad makamo mkuu wa taaluma katika kituo cha faharasi, semina hiyo itadumu kwa muda wa siku (12) imepata mwitikio mkubwa”.

Kumbuka kuwa nadwa, warsha na semina zinazo fanywa na maktaba pamoja na Daaru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya ni moja ya njia ya kuimarisha uhusiano na maktaba zingine pamoja na kubadilishana uzowefu, kituo cha faharasi na kupangilia taaluma ni miongoni mwa vituo vyenye uzowefu mkubwa katika sekta hiyo, kimefungua mlango wa kuwajengea uwezo na kuwaendeleza watumishi wa maktaba kama njia ya kubadilishana uzowefu na vituo vingine, nadwa iliyo fanywa hivi karibuni ni moja ya utekelezaji wa lengo hilo, kutokana na mazingira ya sasa imelazimika kutumia njia ya mawasiliano ya kijamiii na kutoa elimu masafa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: