Multaqal-Qamar: Tunaendelea kujenga uwelewa kielimu na kimaarifa

Maoni katika picha
Shekh Haarith Daahi mkuu wa kituo cha Multaqal-Qamar kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, amesema kuwa Multaqa yetu inaendelea kujenga uwelewa na maarifa katika jamii, na kuilinda na aina zote za hatari zinazo izunguka kidini na kijamii, kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii baada ya kushindikana kukutana na walengwa moja kwa moja kutokana na kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Korona.

Akaongeza kuwa: “Tulianza harakati zetu tangu siku za kwanza lilipo tangazwa janga la Korona, tumeendelea hadi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na tumeandaa ratiba kamili yenye vipengele vingi, pamoja na mazingira ambayo taifa linapitia tumeweza kutumia muda tuliopata kwa kusoma Quráni na kufanya tafiti”.

Akaendelea kusema: “Pamoja na hayo; washiriki wa program ya Multaqal-Qamar wanaendelea na harakati za kielimu na kibinaadamu, wanachangia ujenzi wa nchi na wanakusanya vitu kwa ajili ya kusaidi familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika mwezi huu mtukufu, sambamba na kusaidia sekta ya afya kwa kutengeneza barakoa na kushiriki katika shughuli za kupuliza dawa pamoja na shughuli zingine”.

Akabainisha kuwa: “Tumefanya mashindano ya kielimu yaitwayo, watambue viongozi wa kitamaduni na kitaifa wa Iraq, washiriki walitakiwa kuandika Makala kuhusu mtu makhsusi, watu walio teuliwa ni (Dkt. Hussein Ali Mahfuudh na Shekh Shahidi Mushtaqu Zaidi) kila mshiriki alipewa wiki moja kuandika kuhusu watu hao, ili kutoa nafasi ya kuuliza kuhusu watu hao na urithi wao hapa Iraq, ushiriki ulikua mzuri, tumekusanya makumi ya Makala”.

Akaendelea kusema: “Hali kadhalika tumeendesha mashindano kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii, lengo letu lilikuwa ni kudumisha mawasiliano kati ya vijana wa kiiraq, hususan walio shiriki katika mafunzo yetu siku za nyuma mwaka (2018 na 2019), tumechagua kitabu cha (Albayaanu fi tafsiiril-Quráni) cha Sayyid Abu Qassim Khui kwa ajili ya shindano la wiki hii, kupitia program ya (Iqra-a maál-qamar)”.

Tambua kuwa unaweza kushiriki katika harakati zote kupitia mitandao yetu ya kijamii au kwa kutumia namba ya simu ifuatayo (009647726563473).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: