Kwa ufuatiliaji wa washiriki zaidi ya (570) kutoka ndani na nje ya Iraq: chuo kikuu cha Alkafeel kimeratibu mhadhara kuhusu fizikia ya hesabu

Maoni katika picha
Idara ya elimu endelevu kwa kushirikiana na mchepuo wa udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeendesha ratiba ya kutoa mihadhara ya kielimu kwa kutumia intanet kuhusu fizikia ya hesabu kwa kutumia program ya (The Cardiovascular system and Exercise).
Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Hussein Albakaa: “Mhadhara uliendeshwa kwa kufuata maelekezo ya uongozi wa chuo chini ya rais wa chuo Dokta Nusir Dahani, sambamba na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu kuhusu umuhimu wa kunufaika na kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, na kuendeleza mawasiliano ya kielimu na tafiti, mihadhara hii ni sehemu ya mihadhara mbalimbali iliyo ratibiwa na chuo”.

Akaongeza kuwa: “Mhadhara huu umefuatiliwa na zaidi ya watu (570) ambao ni wakufunzi wa vyuo kutoka ndani na nje ya Iraq, tumeongelea mambo mengi ikiwa ni bamoja na kubaini kasi ya mapigo ya moyo katika mazingira ya utulivu, na mapigo ya moyo yanayo kwa kila umri wakati wa mazowezi (Maximum heart rate) pamoja na kuangalia athari za pembeni, kama vile uzito, kiwango cha damu, mafuta yanayo athiri damu (LDL)”.

Akabainisha kuwa: “Mwishoni mwa mhadhara vikaongelewa vipengele muhimu kwa ufupi, ikiwa ni pamoja na kusisitiza umuhimu wa mazowezi katika maisha ya mwanaadamu kwa ajili ya kujiepusha na maradhi kupitia mazowezi”

Kumbuka kuwa idara ya elimu endelevu kwa kushirikiana na vitengo vya chuo kikuu wanafanya mihadhara mbalimbali kwa njia ya mtandao, na kuendelea kujenga uwezo wa wakufunzi wa vyuo kielimu na kitafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: