Mradi wa Firdaus umekamilisha uvunaji wa dunam (400) za ngano

Maoni katika picha
Idara ya mradi wa kilimo Firdaus chini ya shirika la Liwaau katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kumaliza msimu wa uvunaji wa ngano aina ya (Buhuth 22) katika shamba la umwagiliaji wa maji ya visima lenye ukubwa wa dunam (400).

Mhandisi Aadil Maliki aliuambia hivyo mtandao wa Alkafeel, akaongeza kuwa: “Baada ya kumaliza kujiandaa kwa ajili ya msimu wa mavuno ya ngano zilizo limwa eneo hilo kwa mara ya kwanza kufuatia mkakati wa kilimo wa mkoa wa Karbala, tukaanza kazi ya kuvuna ambayo imeenda vizuri, kisha mazao tuliyo vuna tumeyaweka kwenye magodauni ya wizara ya kilimo ya Iraq yaliyopo Karbala yaliyo kuwa yameandaliwa kwa ajili ya nafaka hizo”.

Fahamu kuwa eneo lote la shamba lilisamadiwa, sambamba na kumwagiliwa na shirika la teknolojia ya kilimo Khairul-Juud, kupitia pembejeo za shirika hilo tumepata mafanikio makubwa ukilinganisha na mashamba mengine, hakika tumepata mavuno makubwa tofauti na wengine.

Kumbuka kuwa kwa kumaliza uvunaji huu Atabatu Abbasiyya inakuwa imemaliza kazi ya uvunaji katika mwaka huu, ambapo ilikuwa ina sehemu tatu ikiwemo sehemu ya Firdausi ambayo ni:

Shamba la Saaqi: lenye ukubwa wa dunam (480) lililopandwa aina bora kabisa ya ngano ambayo ni, aina ya (Bagdad) iliyo pandwa kwenye shamba lenye ukubwa wa dunam (360) na aina ya (Buhuthu/22) iliyo pandwa sehemu yenye ukubwa wa dunam (480).

Sehemu ya shamba la kumwagilia ilikuwa na ukubwa wa zaidi ya dunam (400), ngano iliyo vunywa ni aina ya (Buhuthu/22) na (Al-Ibaa/99), hali kadhalika tumevuna shairi aina ya (Shairi244) na (Shairi9/12).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: