Iraq imeingizwa katika ripoti ya (IFLA) kupitia maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Muungano wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) umeiingiza Iraq kupitia maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kwenye ripoti maalum ambayo wametoa hivi sasa kuhusu mchango wa maktaba katika kupambana na tatizo la maambukizi ya virusi vya Korona.

Tumeongea na Ustadh Saamir Baasim makamo mkuu wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma, amesema: “Muungano wa kimataifa wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) unajumla ya nchi wanachama (150) ikiwemo Iraq ambayo inawakilishwa na maktaba pamoja na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, kutokana na mazingira ya sasa ya kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona, muungano huo umeorodhesha maktaba ambazo zimechangia kupunguza maambukizi ya virusi hivyo katika shughuli zao na kutumia mfumo wa kutoa huduma kwa njia ya mtandao (huduma masafa) sambamba na kuendelea kutoa huduma bila kusimama”.

Akasema: “Kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona kumesababisha taasisi nyingi za maktaba katika nchi nyingi kufunga shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kufunga maktaba, lakini maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya haikufunga shughuli zake, bali iliongeza shughuli ya uendeshaji wa nadwa na kubadilishana fikra sambamba na kujenga uwelewa kwa watumishi, wala hawakuishia kufanya nadwa peke yake, bali shughuli zote za maktaba zimeendelea, ikiwa ni pamoja na kuendesha semina kwa watumishi wa maktaba na zinginezo”.

Kumbuka kuwa maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya imeendelea kufanya kazi kwa tahadhari na kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, imetumia njia za kisasa na kimtandao katika shughuli zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: