Watumishi wa Abbasi wamefika katika wilaya ya Badrah mkowani Waasit na kupuliza dawa

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wanaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Waasit kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kazi hiyo inaendelea katika wilaya ya Badrah, wamepulizia nyumba za makazi ya watu, mitaa na kwenye majengo ya taasisi za serikali.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: “Wamepuliza maeneo mbalimbali katika wilaya ya Badrah, kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na Maukibu ya Imamu Hujjah (a.f) kwa ajili ya kuwalinda wakazi wa wilaya hiyo kutokana na maambukizi ya virusi vya Korona, hususan baada ya kutokea kisa cha maambukizi katika wilaya hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Wanafanya hivyo kutokana na maagizo ya Marjaa Dini mkuu ambayo yanahimiza kufuata maelekezo ya idara ya afya, aidha ni sehemu ya opresheni maalum ya kikosi cha Abbasi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Sha’abi) kimesha fanya kazi ya kupuliza dawa kwenye mikoa tofauti hapa nchini na bado kinaendelea na kazi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: