Waziri wa afya ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia kazi zinazo fanywa na Ataba katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Waziri wa afya na mazingira Dokta Hassan Tamimi ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kufanya ibada ya ziara na kusoma dua akapokewa na Katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, jioni ya siku ya Ijumaa mwezi (28 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (22 Mei 2020m) kwenye ziara aliyo fanya katika mkoa wa Karbala ya kuangalia hatua zinazo chukuliwa kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na maandalizi yaliyo fanywa katika hospitali ya Imamu Hussein (a.s) –iliyokuwa inajulikana kama hospitali ya Turki siku za nyuma-.

Waziri ameongozana na mkuu wa mkoa wa Karbala Ustadh Jaasim Khatwabi pamoja na muwakilishi wa diwani Shia katika mambo ya kitaalam, na mkuu wa idara ya afya katika mkoa wa Karbala pamoja na mkuu wa mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, na msemaji wa wizara ya afya.

Waziri pamoja na ujumbe aliofuatana nao wameangalia shughuli za kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katibu mkuu akaeleza kwa ufupi kazi zinazo fanywa na Ataba katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, kuanzia ndani ya Ataba hadi jinsi inavyo saidia sekta ya afya kwa kujenga kituo cha Alhayaat katika mji wa Imamu Hussein (a.s) na kile kilicho jengwa katika hospitali kuu ya Hindiyya, ikiwa ni pamoja na kazi ya kupuliza dawa barabara za Karbala, sambamba na barakoa pamoja na dawa zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud na kuzigawa katika taasisi za afya na kwa wananchi, pamoja na mambo mengine mengi yanayo husiana na swala hilo.

Mwisho waziri akaagwa kama alivyo pokelewa, akapongeza na kushukuru kazi zinazo fanywa na Ataba tukufu katika kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa hii ni ziara ya kwanza ya waziri wa afya katika mkoa wa Karbala tangu apewe madaraka hayo, ametembelea pia Atabatu Husseiniyya na idara ya afya ya mkoa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: