Kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kulinda nidamu katika Atabatu Abbasiyya wanafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru ndani ya siku hizi za Mwezi mtukufu wa Ramadhani, wana mkakati maalum wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Haidari Majhuul Muhammad amesema kuwa: “watumishi wa kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Abbasiyya kila mwaka ndani ya mwezi wa Ramadhani hufanya kazi kubwa ya kuwahudumia mazuwaru, lakini mwaka huu kuna jambo la tofauti na miaka mingine nalo ni kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, katika mazingira haya magumu, tumeweka mkakati maalum unao kidhi maelekezo yaliyo tolewa na sekta za afya, kuanzia katika Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na maeneo yote ya mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wanapulizia dawa milango ya haram tukufu muda wote saa (24), ili kuweka mazingira salama kwa mazuwaru wanao ingia na kutoka sambamba na kuwafanyia upekuzi kama kawaida, mazuwaru wanakaribishwa chini ya kanuni na maelekezo ya idara ya afya ya kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha fanya mambo mengi kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ilianza kuchukua hatua mara tu baada ya kutangazwa kuwepo kwa virusi hivyo.

Shughuli zinazo fanywa pamoja na juhudi kubwa iliyopo inatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata muongozo wa idara ya afya, pia ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: