Ataba yatangaza kutokuwepo kwa swala ya Idi

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kuwa hakutokuwepo na swala ya Idi kwa sababu za mazingira ya kiafya ambayo taifa la Iraq linapitia.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya idara ya afya ya mkoa wa Karbala, na kufuatia kuheshimu maelekezo hayo tangu yalipo tolewa tunatangaza kuwa hakutakuwa na swala ya Idi mwaka huu 1441h”.

Akabainisha kuwa: “Maamuzi haya yametokana na mazingira ya afya ya sasa na kuheshimu maelekezo ya sekta ya afya katika mkoa mtukufu wa Karbala, ambayo yamezuwia mikusanyiko mikubwa ya watu”.

Kumbuka kuwa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zilitoa tamko la kusimamisha swala za jamaa tangu mwezi (15 Rajabu 1441h) sawa na (11 Februari 2020m) kutokana na maelekezo ya idara ya afya, ili kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.

Tambua kuwa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani alijibu swali lililo elekezwa katika ofisi yake kuhusu hukumu ya kuswali jamaa katika mazingira ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Swali lilikuwa ninasema: Ni ipi rai ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu kuhusu kushiriki kwenye swala ya jamaa katika siku hizi ambazo yanashuhudiwa maambukizi ya virusi vya Korona?

Akajibu: kwa kuwa mikusanyiko ya watu imepigwa marufuku kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, inatakiwa kuheshimu marufuku hiyo na kuifanyia kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: