Muhimu.. ofisi ya Marjaa Dini mkuu imetangaza kuwa: Siku ya Jumapili tunakamilisha mwezi wa Ramadani na siku ya Jumatatu 25 Mei ndio siku ya kwanza Idil-fitri tukufu.

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu imetangaza kuwa, kesho siku ya Jumapli tunakamilisha mwezi wa Ramadhani na siku ya kwanza ya Idil-fitri sawa na mwezi mosi Shawwal 1441h itakua siku ya Jumatatu sawa na (25 Mei 2020m).

Lifuatalo ni tamko maalum lililotolewa na ofisi:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani katika mji wa Najafu inawatangazia waumini watukufu, haujathibiti mwezi muandamo baada ya kuzama jua leo siku ya Jumamosi (29/ Ramandani 1441h), wala huijathibiti kuonekana mwezi kwa macho hapa Irad na maeneo ya jirani ya Iraq, unatarajiwa kuonekana kesho ukiwa juu na kwa uwazi zaidi, hilo sio dalili kuwa ni mwezi wa siku mbili. Fatwa ya Mheshimiwa Sayyid inasema kuwa, mwanzo wa mwezi katika kila nchi unatokana na kuonekana mwezi muandamo kwa macho moja kwa moja wala sio kwa kutumia vifaa au kuonekana kwenye nchi zingine duniani, hivyo kesho tunakamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, siku ya Jumatatu itakuwa ndio siku ya kwanza ya Idil-fitri.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu awakubalie ibada zenu na tunakutakieni sikukuu yenye kheri na baraka wa waislamu wote hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.

Kumbuka kuwa kituo cha tafiti za anga ambacho kipo chini ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani kilitoa taarifa inayo zungumzia uwezekano wa kuonekana mwezi muandamo wa Shawwal kwa macho, isemayo kuwa:

Hakika mwezi muandamo wa Shawwal –kwa mujibu wa tafiti za kielimu zilizo fanywa na kituo cha tafiti za anga-, utaonekana kwa macho dunia nzima baada ya kuzama jua la siku ya Jumapili (24/ 05/ 2020m).

Utafiti wa kielimu unaonyesha kuwa siku ya (Jumamosi 29 Ramadhani 1441h) kuna maeneo (60) ambazo ni vigumu kuonekana mwezi muandamo kuanzia mji wa Sidni mashariki mwa Australia hadi mji wa Wait, Kanada magharibi, maeneo yote ya mashariki ya kati pamoja na Ulaya hautarajiwi kuonekana.

Maeneo ya afrika wanamazingira bora ya kuona mwezi muandamo tofauti na mashariki ya kati, nchi za magharibi ya Afrika zina nafasi nzuri zaidi ya kuona mwezi dofauti na nchi zingine za Afrika.

Maeneo yenye nafasi zuri zaidi ya kuona mwezi siku ya Jumamosi ni Marekani ya kati.

Hii ni kwa mujibu wa hali ya anga na uzowefu wa muandamo wa mwezi kwenye maeneo hayo.

Tambua kuwa baadhi ya wasomi na watafiti wanakubali mwezi muandamo wa kuona kwa kutumia vifaa, aidha wanasema inawezekana ukaonekana kwa macho moja kwa moja baada ya kuzama jua la siku ya Jumamosi katika nchi za mashariki ya kati na Ulaya.

Tutapokea taarifa za kuandama kwa mwezi na kuziwasilisha katika kamati ya kisheria; kwa sababu mwanzo wa mwezi muandamo hautegemei hesabu za kielimu peke yake, bali unategemea pia kuthibiti kisheria muandamo wa mwezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: