Maoni katika picha
Zimesikika sauti muruwa za wasomaji, zinazo tia hisia ya huzuni kwa msikilizaji kutokana na kuuaga mwezi huu mtukufu, kama ulivyo pokewa na minara miwili mitakatifu, mnara wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), leo unaagwa kwa maneno yanayo tia huzuni, tunamuomba Mwenyezi Mungu aurejeshe tena kwa waumini mwakani, mazingira halisi yanasema: Mwezi wa Ramadhani jua lake limekaribia kuzama, saa zake zimeisha na siku zake zimeondoka, tunauaga huenda ikawa ndio mara ya mwisho, na huenda tukakutana nao mwakani kama Mwenyezi Mungu akituandikia hivyo, alikuwa ni mgeni mwenye siku za kuhesabika, siku hizo zimeisha haraka.
Miongoni mwa beti zilizo sikika zikisomwa kwenye minara ya malalo mawili takatifu ni:
Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa Ramadhani
Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa kisimamo
Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa twaa na ghufraan
Kwaheri kwaheri ewe mwezi wa wema na ihsaan