Eneo la katikati ya haram mbili tukufu: kazi ya usafi inaendelea muda wote

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanafanya kazi kubwa ya kusafisha uwanja wa katikati ya malalo mbili takatifu na sehemu iliyo pauliwa, wanafanya usafi wa aina tofauti, kuna wanao husika na mapambo pamoja na kupanda miti, wengine wanahusika na umeme na wengine wanafagia na kupiga deki, kila kazi ya kundi fulani ni sehemu ya kukamilisha kazi ya kundi lingine, jambo hilo linamfanya mtu anayekuja kufanya ziara aone eneo hilo ni sehemu ya malalo hizo takatifu.

Haya ndio yaliyo semwa kwa ufupi na rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi, akaongeza kuwa: “Tunafanya kazi kila siku, kazi zetu huongezeka wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu na mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na uchache au kutokuwepo kwa mazuwaru kwa sababu ya tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, lakini kazi zetu zinaendelea bila kusimama, kufuatia kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya”.

Miongoni mwa idara zenye kazi kubwa ni idara ya utumishi, tumeongea na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Ahmadi Ali Kaadhim amesema kuwa: “Idara ya utumishi ni miongoni mwa idara muhimu katika kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu, inajukumu la kudumisha usafi kwenye uwanja huoa na eneo lililo pauliwa, baada ya kuingia balaa la virusi vya Korona tumeongeza kazi tezu kwa ajili ya kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama”.

Akaongeza kuwa: “Tunafanya kazi usiku na mchana kwa kutumia vifaa vilivyo elekezwa na idara ya afya, sawa tuwe tunatumia mikono au mitambo, sambamba na kazi hiyo tunasafisha pia barabara zinazo elekea kwenye malalo mbili takatifu na sehemu za pembezoni mwake, pamoja na kusafisha vituo vya maji ya mvua na sehemu za vyooni”.

Akasisitiza kuwa: “Kutokana na maelekezo yaliyo tolewa na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumechukua tahadhari zote za kuwalinda watumishi wetu dhidi ya maambukizi ya Korona na kuhakikisha usalama wao, tumepunguza idadi ya watumishi katika kila kazi, pamoja na kuwapulizia dawa kila wanapo maliza kazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: