Majina ya washindi wa shindano la kijana wa Alkafeel lililo fanywa ndani ya mwezi wa Ramadhani na kushiriki zaidi ya wanafunzi (1000)

Maoni katika picha
Kamati iliyokuwa inasimamia shindano la kijana wa Alkafeel lililofanywa kwa njia ya mitandao ndani ya mwezi wa Ramadhani na kuwahusisha wanafunzi wa vyuo na shule za Iraq imetangaza majina ya washindi, shindano hilo lilikuwa sehemu ya kukumbuka kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), lilifanywa mwezi 22 Ramadhani.

Kiongozi wa idara ya harakati za chuo Ustadh Muntadhir Swadiq amesema kuwa: “Jumla ya wanafunzi (1033) kutoka vyuo na shule mbalimbali hapa Iraq wameshiriki kwenye shindano hilo, majibu sahihi yalikuwa (650), ikabidi tupige kura ili kupata washindi kumi wa mwanzo, kura hiyo ilifanywa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Idil-fitri”.

Akasema: “Washindi watapewa zawadi za kutabaruku kutoka ndani ya Atabatu Abbasiyya pamoja na vyeti vya ushiriki, sambamba na zawadi zingine watapewa wale waliojibu vizuri kwenye shindano hilo”.

Akaendelea kusema: “Majina yaliyo faulu baada ya kupiga kura ni:

Kwanza: Zainabu Yahya Halul kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya Bagdad.

Pili: Muhammad Ali Hassan kutoka kitivo cha uuguzi chuo kikuu cha Karbala.

Tatu: Qamar Abbasi kutoka shule ya Swiraat Najafu Ashrafu.

Nne: Ahmadi Qassim Shakuur kutoka shile ya Nail katika mkoa wa Swalahu-Dini.

Tano: Hussein Muayyad kutoka I’daya-Khidhri (a.s) katika mkoa wa Muthanna.

Sita: Maitham Muhammad Aribi kutoka kitivo cha uhandisi chuo kikuu cha Bagdad.

Saba: Dhuha Abbasi Haadi kutoka shule ya wasichana ya Hauraa (a.s) katika mkoa wa Karbala.

Nane: Rifaa Jaabir Muhajir kutoka kitivo cha tarbiyyah chuo kikuu cha Basra.

Tisa: Zaharaa Aadil Shanani kutoka shule ya Halwaan katika mkoa wa Najafu.

Kumi: Ahmadi Rasuul Shamkhi kutoka shule ya Ibun Sina katika mkoa wa Qadisiyya.

Kumbuka kuwa shindano hili lilitangazwa kwenye mtandao, lilikuwa na maswali ishirini, na usahihishaji wa majibu ulifanywa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: