Idi ni ya nani?

Maoni katika picha
Siku ya kwanza katika mwezi wa Shawwal ni siku inayo hitimisha safari ya waislamu ya kuvuna thawabu na rehma, katika siku za mwezi wa Ramadhani usingizi wao ulikuwa ni ibada, pumzi zao waliandikiwa thawabu za tasbihi, muislamu anakua na furaha mbili kubwa. Kwanza: kumaliza mwezi wa ibada. Pili: furaha ya kuwa na uhakika wa kupata malipo mema, Mtume (s.a.w.w) ameiita siku hiyo kuwa ni siku ya malipo, siku ambayo hulipwa yule aliye funga na akaswali.

Katika siku hiyo waumini husalimiana na kupongezana kwa kumaliza siku tukufu ambazo wamevuna fungu kubwa la hazina ya akhera, nafsi hutulia na nyoyo hufurahi, waumini huendelea kutendeana wema na nyoyo zao hutakata kutokana na chuki.

Kwa hiyo sio siku ya michezo na upuuzi, ni siku ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake na neema zake.

Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib –a.s- katika siku ya Idil-Fitri alisema: “Enyi watu hakika siku ya leo wanalipwa walio fanya wema na wanapata hasara wasio tenda wema, inafanana na siku ya kiyama, mnapo toka nyumbani kwenda kuswali kumbukeni mtakavyo toka makaburini kwenda mbele ya Mola wenu, mtakapo simama kuswali, kumbukeni kisimamo chenu mbele ya Mola wenu, mtakapo kuwa mnarudi majumbani kwenu kumbukeni nyumba mtakazo kwenda siku ya kiyama”.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu jambo dogo zaidi wanalopata watu waliofunga wakiume na wakike, wataitwa na malaika katika siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani na kuambiwa, nakupeni bishara njema enyi waja wa Mwenyezi Mungu mmesamehewa dhambi zenu mlizo kuwa nazo, angalieni mtafanya nini katika siku zijazo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: