Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) imetoa kitabu cha sira cha nne

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa vitabu vya sira, Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) ndani ya kituo cha utafiti Al-Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa kitabu cha nne kiitwacho: (Mwenendo wa mapokezi ya sira ya Ibun Hisham: kufuatia habari na matukio ya kitamaduni), kilicho andikwa kama kazi ya shahada ya masta ya mtafiti Ghanim Hamidi Zubaidi, ambae alikuwa mshindi wa tatu kwenye shindano la kimataifa la wanafunzi wa vyuo lililo endeshwa na Daru Rasuul Aádham.

Sira ya Mtume iliyo andikwa na Muhammad bun Is-haqa Matlabi (aliyekufa mwaka 218h, sawa na 833m, au 213h sawa na 828m) na kujulikana kwa jina la “Sira ibn Hisham”.

Sira ya Mtume mtukufu ni moja ya rejea muhimu katika utamaduni wa kiarabu na kiislamu baada ya Quráni, imejaa matukio muhimu ya kihistoria, kimaadili na kisheria, maisha ya Mtume (s.a.w.w) yamejaa mafundisho muhimu ya kiroho kwa kila muislamu, tambua kuwa matendo yake ni msingi wa pili wa sheria ya kiislamu, kwa hiyo kuna uhisiano wa kiroho kati ya sira yake na waislamu, ambapo waislamu wanatakiwa kumfuata Mtume kiitikadi, kitabia na mwenendo wote kwa ujumla.

Tambua kuwa Daru imebeba jukumu la kuchapisha kila kitu kinacho muhusu Mtume (s.a.w.w) na kufanya jambo hilo kuwa sehemu ya harakati yake kielimu na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: