Idara ya utumishi inaendelea na kazi katika kitengo cha Maqaam

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha Maqaam ya Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) wanaendelea na kazi ya kufanya usafi katika eneo hilo, pamoja na kwenye soko la Imamu Swadiq (a.s) lililopo karibu na Maqaam hiyo, miongoni mwa watumishi hao ni wale wa idara ya utumishi.

Kiongozi wa idara ya utumishi katika Maqaam Ustadh Swahibu Azizi Hassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara yetu inamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu hayo ni kudumisha usafi sehemu ya ndani ya Maqaam kwa kufagia na kupiga deki pamoja na maeneo yote yanayo izunguka, sambamba na kusafisha soko la Imamu Swadiq (a.s), kazi hiyo hufanywa kwa kutumia mitambo maalum”.

Akaongeza kuwa: Aidha ni jukumu letu kuwapa maji ya kunywa mazuwaru, kwa kuweka maji kwenye mahodhi na madeli, na kwenda kusafisha mazulia na kutandika mengine masafi.

Akaendelea kusema: “Kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, tumepewa jukumu lingine, kila siku tunafanya kazi ya kupuliza dawa sehemu zote zinazo zunguka Maqaam tukufu”.

Tambua kuwa kitengo cha Maqaam ya Imamu Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kuwa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya unapo ingia Karbala kwa upande wa kaskazini kupitia eneo la mlango wa Salama, Maqaam inakuwa mbele yako katika barabara ya Sidra, mkabala na haram ya Imamu Hussein (a.s) kushoto, ipo umbali wa mita (650) takriban, nayo ni miongoni mwa Maqaam muhimu sana katika mji mtukufu wa Karbala, kutokana na kufungamana kwake na Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: