Chuo kikuu cha Alkafeel kimepata nafasi ya sita katika mfumo wa kimataifa wa (Scopus)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimepata nafasi ya sita katika vyuo vikuu binafsi vya Iraq chini ya mfumo wa (Scopus) kwa mwaka 2019m.

Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chuo kimepata nafasi hii baada ya kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ya umuhimu wa kujali tafiti za kielimu zinazo saidia jamii kutatua changamoto za sekta ya viwanda, kilimo na mazingira, chuo kimeweka mazingira mazuri kwa kila anayetaka kufanya utafiti, kwa kuandaa na kutangaza tafiti zao katika majarida ya kimataifa, kuingia kwa chuo katika mfumo wa (Scupos) na (Clarivate) ni mwanzo wa kuelekea kwenye mfumo wakisasa zaidi siku za mbele”.

Akafafanua: “Mkakati wa chuo unashajihisha wasomi kufanya tafiti za kielimu na kutangaza matokeo ya tafiti zao katika jamii”.

Akaongeza kuwa: “Chuo kimepata nafasi hiyo katika vyuo binafsi (64) vya hapa Iraq, huku vyuo (32) vikifanikiwa kuingia katika mfumo wa (Scopus)”.

Akasisitiza kuwa: “Chuo kinaendelea na utaratibu wa kushiriki katika mambo ya kimataifa”.

Kumbuka kuwa mfumo wa (Scopus) ni miongoni mwa mifumo ya kimataifa ya kisasa, aidha ni matokeo ya sanifu za majarida ya kimataifa yanayo andika tafiti tofauti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: