Kwa ushiriki wa zaidi ya watu (250) kwenye shindano: yametangazwa majina ya washindi wa shindano la (Rawaafid) linalo husu turathi za kiislamu

Maoni katika picha
Kamati iliyokuwa inasimamia shindano la (Rawaafid) la turathi za kiislamu kwa njia ya mtandao kitengo cha wanawake imetangaza majina ya washindi.

Shindano hilo liliendeshwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa ajili ya kueneza uwelewa wa kitamaduni na kujenga moyo wa kushindana katika mambo ya sanaa yanayo saidia kutufanya tuzijali turathi zetu za Iraq na kutujenga kwa mustakbali.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekh Ali Asadi akasema: “Baada ya kupokea majibu ya washiriki na kuchambua majibu sahihi kisha kupigiwa kura matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza ni Sara Haadi Mahmud Alhasani.

Mshini wa pili ni Ali Turki Hashushu Alfatalawi.

Mshindi wa tatu ni Zainabu Jamili Kadhim Ibrahim”.

Akafafanua kuwa: “Zawadi watakazo pewa washindi ni:

Mshindi wa kwanza/ Msahafu mtukufu na kitabu cha (Jawaamii Jaamii) pamoja na pete ya fedha kutoka katika baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mshindi wa pili/ Kitabu cha (Turathi za Karbala) pamoja na pete ya fedha kutoka katika baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mshindi wa tatu/ Majarida yanayo elezea mambo ya kitamaduni pamoja na pete ya fedha kutoka katika baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: