Waziri wa mambo ya ndani ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na katibu mkuu

Maoni katika picha
Waziri wa mambo ya ndani wa Iraq Luteni Jenerali Othumani Ghanimi akiwa na viongozi wa maafisa usalama wa mkoa wa Karbala baada ya Adhuhuri ya leo (2 Shawwal 1441h) sawa na (26 Mei 2020m) ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumaliza ibada ya ziara na dua amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar akiwa na makamo wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi.

Wamejadili mambo mengi ikiwa ni pamoja na hatua zinazo chukuliwa na Ataba tukufu za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na ujenzi uliofanywa hivi karibuni wa vituo viwili vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona na kuvitoa zawadi kwa idara ya afya ya mkoa wa Karbala, sambamba na kusaidia miradi mingi ya afya, bila kusahau kazi kubwa inayo fanywa na shirika la Khairul-Juud ya kutengeneza barakoa na kuzigawa kwa wananchi na kwenye vituo vya afya, wakajadili pia maswala ya usalama kwa ujumla katika mkoa wa Karbala na kwa namna ya pekee katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mwisho wa kikao hicho waziri alisifu na kupongeza kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya afya na usalama pamoja na sekta zingine, halafu akaagwa kwa bashasha kama alivyo pokelewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: