Mkuu wa kikosi cha Abbasi amesema kuwa: Mradi wa nyumba za makazi Alwafaa umetekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mradi wa nyumba za makazi ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Alwafaa, umetekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha usimamizi wa kihandisi kwa ajili ya kuzipatia familia za mashahidi na majeruhi nyumba za makazi.

Yamesemwa na kiongozi mkuu wa kikosi Ustadh Maitham Zaidi kwenye ufunguzi wa nyumba hizo: “Kiwanja kilicho jengwa nyumba hizi kimetolewa na moja ya familia za Karbala, na mradi umetekelezwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pesa zimetoka kwa Marjaa Dini mkuu kupitia muwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akafafanua kuwa: “Mradi huu inaitwa (Nyumba za makazi Alwafaa wa kwanza) hii ni hatua ya kwanza ya ujenzi wa nyumba zingine”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumanne mwezi (2 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (26 Mei 2020m) imefanya ufunguzi wa mradi wa Alwafaa ambao ni nyumba za makazi za familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji zilizo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Ataba tukufu.

Tambua kuwa mradi huu ni sehemu ndogo ya kuonyesha kujali kazi kubwa iliyo fanywa na mashahidi watukufu katika taifa hili, na kusaidia familia zilizo kubali kujitolea wapenzi wao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq, wananchi wake na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: