Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo Karbala inakituo cha upasuaji wa moyo kwa watoto, huduma zake zinafanana na zile zinazo tolewa na haospitali kubwa zilizopo kwenye nchi zilizo endelea katika kiwango cha upasuaji wa moyo, kituo kinamiliki vifaa tiba vya kisasa, ikiwa ni pamoja na moyo wa kutengenezwa, ambao huwekwa sehemu ya moyo wakati wa kufanya upasuaji.
Kiongozi wa upasuaji wa moyo Dokta Ahmadi Abudi amesema kuwa: “Hakika kituo cha upasuaji wa Moyo kwa watoto katika hospitali ya rufaa Alkafeel, pamoja na uchanga wake kinatoa ushindani mkubwa kwa vituo vya aina hiyo vilivyopo katika nchi zilizo endelea, kutokana na vifaa ilivyo navyo pamoja na madaktari bingwa na wauguzi wenye weledi mkubwa”.
Akabainisha kuwa: “Hakika kituo hiki ni mbadala bora kwa wagonjwa waliokua wanakwenda nchi za nje kutafuta matibabu”.
Akasema: “Miongoni mwa vifaa tiba muhimu vilivyopo katika kituo hicho ni moyo wa kutengenezwa, unao fanya kazi ya moyo wakati wa upasuaji”.
Akafafanua kuwa: “Moyo una pampu mbili, moja ya kuingiza na nyingine ya kutoa na kuna kifaa cha kuendesha pambu hizo, na kingine kinapangilia msukumo wa pampu”.
Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel daima hujitahidi kufanya upasuaji kisasa kutokana na vifaa tiba bora ilivyo navyo, sambamba na umahiri wa madaktari wake kuanzia wazawa na wageni, jambo ambalo limeifanya kuchuana na hospitali kubwa za kimataifa.
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hupokea madaktari bingwa wa fani mbalimbali kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote walio katika hali zote.