Zaidi ya mazuwaru elfu (95) wamefanyiwa ziara kwaniyaba ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel, ambao ni toghuti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya ibada ya –ziara na swala- pamoja na kusoma dua maalum ya ziara zilizo fanywa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani sambamba na kufanya baadhi ya ibada maalum kwa ajili ya watu walio jisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niyaba.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir kiongozi wa idara ya taaluma na mitandao iliyo chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu: “Idadi ya watu ambao wamefanyiwa ziara kwa niyaba na mtandao imefika (95381) kutoka nchi tofauti duniani, kupitia mitandao yetu yote (wa Kiarabu – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Kiurdu – Kifaransa – Kiswahili – Kijerumani)”.

Akaongeza kuwa: “Kulikua na zaidi ya aina moja ya ziara ndani ya mwezi huu mtukufu, kulikuwa na ziara zifuatazo:

  • - Ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku pamoja na kufanya baadhi ya ibada maalum za mwezi wa Ramadhani, jukumu hilo lilifanywa na idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Ataba takatifu na walikuwa wanafanya kila siku jioni.
  • - Ziara ya Imamu Hassan (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, jukumu hilo lilifanywa na watu walio jitolea katika mji wa Madina Munawwarah.
  • - Ziara ya kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, nayo ilifanywa na baadhi ya watumishi wa malalo hiyo takatifu katika mji wa Najafu Ashrafu.
  • - Ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Idil-Fitri na mchana wake, ilifanywa na idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema: “Kulikuwa na muda mrefu wa kutangaza ziara hizo, na kutoa fursa ya kushiriki idadi kubwa zaidi, asilimia kubwa ya watu walio jisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Moroko, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Aljeria, Afughanistan, Oman, Ekowado, Brazil, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Finland, China, Ealend, Hong Kong, Japani, Falme za kiarabu, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: