Mkufunzi wa warsha hiyo ni (Dkt. Taqi bun Abduridhwa Abduwani) kutoka Oman, katika warsha hiyo watajadili changamoto kubwa zinazo patikana vyuoni, na mambo ya baadae au utafiti wa mustakbali, pamoja na athari za teknolojia katika soko la ajira, watajadili pia tafakari ya aina sita katika kuandaa mkakati wa chuo wa kujihami na hatari zisizo julikana.
Usajili uko wazi kwa watu wafuatao:
- - Marais wa vyuo na mawakala wao pamoja na wasaidizi wao.
- - Wakuu wa vitengo na mawakala wao pamoja na wasaidizi wao.
- - Wakuu wa vitivo na idara katika vyuo vikuu vya Iraq.
Kumbuka kuwa tangu kufunguliwa kwa chuo kikuu cha Al-Ameed kimejitahidi kujenga uhusiano mzuri na vyuo vikuu vya kiarabu na kiajemi kutoka nchi mbalimbali, kama sehemu ya kuboresha mitaala ya elimu pamoja na kubadilishana uzowefu.