Aina (6000) za kunazi zinapatikana kwenye shamba la dunam (70): Shamba darasa la kunazi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Shamba darasa la kunazi ni moja ya miradi ya kilimo inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika mfululizo wa miradi ya mashamba ya mfano, kwa lengo la kuendelea kueneza kijani kibichi katika mkoa wa Karbala na kuweka mazingira vizuri pamoja na kupunguza eneo la jangwa, sambamba na kutafuta mbegu adimu na kuzipanda ili kuzifanya ziwe nyingi na zipatikane kwa urahisi hapa Iraq katika siku za mbele.

Kiongozi wa Idara ya shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha mapambo na miti Mhandisi Mustafa Hassan Haadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shamba hili ni sehemu ya mkakati wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya wa kunufaika na baadhi ya maeneo, kwa kulima baadhi ya mazao, kwa lengo la kuongeza kipato cha Ataba na kuifanya iweze kujitegemea”.

Akaongeza kuwa: “Shamba lina ukubwa wa dunam (70) na limepandwa jumla ya aina (5608) za miti ya mikunazi, katika sehemu tano na kila sehemu imepewa jina la mmoja wa As-habu Kisaa (a.s) kama ifuatavyo:

  • - Sehemu ya kwanza (Shamba la Khaatamu Rrusul –s.a.w.w-) linaukubwa wa dunam (11), sehemu hiyo imepandwa aina ya (Ziziphus Mauritiuna) kunazi za Moritania na huitwa kunazi za Tailend, aina hiyo sio maarufu hapa nchini, imeingizwa hivi karibuni, hukua haraka miti yake inamiba midogo na hupamba sana pia matunda yake ni makubwa na mazuri, zinastawi sana katika mazingira ya katikati na kusini mwa Iraq.
  • - Sehemu ya pili (Shamba la Ali bun Abu Twalib –a.s-) linadunam (8) imepandwa aina ya (Ziziphus jujube) kunazi za China, hii ni aina maafuru hapa nchini, inamajani mapana na miba midogo pia matunda yake ni mazuri (yana umbo kama la zaituni) ni nzuri kwa mazingira ya katikati na kusini mwa Iraq.
  • - Sehemu ya tatu (Shamba la Fatuma Zaharaa –a.s-) lina dunam (12) limepandwa kunazi za Mouritania pia.
  • - Sehemu ya nne (Shamba la Imamu Hassan –a.s-) linaukubwa wa dunam (13) limepandwa kunazi za Mouritania.
  • - Sehemu ya tano (Shamba la Imamu Hussein –a.s-) linaukubwa wa dunam (12) limepandwa kunazi za Moritania”.

Akafafanua kuwa: “Shamba linaukanda wa ndani na wa nje, ambao umepandwa kunazi za (kienyeji) na mstari wa miti ya Zaituni ipatayo (230), mstari mwingine una miti ya (Yukabutuzi) kila sehemu tuliyo taja inamiti hiyo, jumla ipo miti (2000), pia kuna mstari wa miti ya miba upande wa mbele ya shamba ipatayo (50)”.

Akasisitiza kuwa: “Asilimia kubwa ya miche iliyo pandwa kwenye mashamba hayo imetoka kwenye vitalu vya Alkafeel, tumechagua aina hizi kutokana na mazingira ya hali ya hewa ya Iraq pamoja na uharaka wa kupamba kwake na namna mauwa yake yanavyo hitajiwa na nyuki, ikumbukwe kuwa moja ya sababu ya kuanzisha kilimo hiki ni kwa ajili ya ufugaji wa nyuki”.

Akaongeza kuwa: “Mradi huu unasamadiwa na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud kwa kutumia mbolea ambayo ni rafiki kwa mazingira, na kuna mfumo wa kisasa wa umwagiliaji”.

Kumbuka kuwa shamba hili lilianzishwa mwaka (2017) katika jangwa lililopo pembeni ya barabara ya Najafu/Karbala, linaendelea kama lilivyo pangwa katika uboreshwaji wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: