Maktaba ya wanawake inaendesha shindano la Makala bora kuhusu janga la Korona duniani

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano la (Makala bora kuhusu janga la Korona duniani), litakalo husisha wanawake pekeyake ambalo ni sehemu ya mashindano ya msimu yanayo lenga (kukuja vipaji na ubunifu).

Kiongozi wa maktaba Ustadhat Asmaa Raád ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Kwa ajili ya kuendeleza mawasiliano ya kielimu na kitamaduni katika mazingira ya sasa ambayo dunia inapitia, kutokana na janga la Korona, na ili kuibua vipaji mbalimbali tumeamua kutumia mazingira haya, tumeandaa mashindano kadhaa, tulianza na shindano la (kutengeneza filamu), na hivi sasa tumetangaza shindano la (Makala bora kuhusu janga la Korona duniani) linalo lenga wanawake peke yao”.

Akaongeza kuwa: “Mshiriki wa shingano hili anatakiwa kuandika mambo yanayo shughulisha dunia kwa sasa kuhusu janga la Korona, kwa kufuata kanuni za uandishi wa Makala, zimeandaliwa zawadi za washindi watatu wa mwanzo, Makala zinatakuwa kuwa na vigezo vifuatavyo:

  • 1- Izungumzie (janga la Korona duniani) peke yake.
  • 2- Izingatie kanuni za uandishi wa Makala kwa kufuata mpangilio (Anuani, Utangulizi, Maudhui, Hitimisho).
  • 3- Maneno yasiwe chini ya (250) na sio zaidi ya (500).
  • 4- Mshiriki asiwe chini ya umri wa miaka kumi na nane (awe mwanamke).
  • 5- Makala iandikwe kwa kutumia program ya (word) na itumwe kwa barua pepe ifuatayo women-library@alkafeel.net na kwenye kitengo cha maktaba katika mtandao wa Alkafeel na ukurasa wa facebook.
  • 6- Ataje majina manne, umri, mkoa na namba ya simu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: