Kikosi cha Abbasi na wizara ya kilimo wamekubaliana kuboresha ndege isiyokuwa na rubani kwa ajili ya ulinzi

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau 26 Hashdi Shaábi) pamoja na ujumbe kutoka wizara ya kilimo wamekubaliana kuboresha ndege mpya isiyokua na rubani kwa lengo la kuitumia kwa ajili ya ulinzi wa mashamba na kupambana na wadudu waharibifu ili kusaidia sekta ya kilimo na wakulima.

Dokta Hussein Saaidiy mjumbe wa kituo cha utafiti na kiongozi wa kitengo cha uboreshaji wa ndege zisizokua na rubani amesema kuwa: Ujumbe kutoka wizara ya kilimo pamoja na uongozi wa kulinda mazao katika idara ya kilimo ya Karbala wametembelea ofisi za kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, wakajadili na wataalamu wa kikosi kuhusu namna ya kuboresha ndege zisizokua na rubani kisha kuzitunia katika kupambana na wadudu waharibifu wa mazao ili kuendelea kunufaika na ndege hizo kama zilivyo tumika kwenye kupambana na nzige katika mkoa wa Muthanna na zikatumika kupuliza dawa katika mkoa wa Karbala.

Akasema kuwa wamekubaliana kuendelea kushirikiana na shirika pamoja na kuziboresha ndege hizo kwa faida ya sekta ya kilimo na wakulima.

Naye Ustadh Samiri Abdu-Razaaq msaidizi wa mkuu wa idara ya kulinda mazao amesema kuwa: Leo tumeangalia ndege zilizo boreshwa katika kikosi, ambazo zipo za aina mbili, kuna ndogo na za saizi ya kati, tunatarajia kuboresha aina nyingine kwa ajili ya kuongeza utendaji na uwezo wa kupambana na wadudu waharibifu.

Akaongeza kuwa aina mpya itazingatia nguvu ya upepo, wizara inauzowefu wa kutumia ndege hizo, kwani imesha wahi kutumia ndege za jeshi la serikali katika kupambana na wadudu waharibifu wa dubaas, uzowefu huohuo ndio tunataka kuutumia katika ndege za kikosi cha Abbasi hususan kwenye maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: