Idara ya Quráni imetangaza kukamilika kwa shindano la hazina za maarifa na kufaulu washindani (66)

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake linalo fungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika shindano liitwalo (hazina za maarifa) lililofanywa kwa njia ya mtandao na kuwahusisha wasichana peke yake, lilikuwa na jumla ya washiriki (570) kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Matokeo ya shindano yalikuwa mazuri ukilinganisha na matokeo ya mashindano mengine, kwa namna washiriki walivyo jibu maswali waliyo ulizwa”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya washindi ni (66), lakini ushindi wa kweli na kupata elimu nzuri iliyokuwepo kwenye shindano hilo”.

Kumbuka kuwa idara ya Quráni kupitia masomo na mashindano inayo endesha kwa njia ya mtandao, inakusudia kujenga tabia ya kutafakari aya za kitabu kitakatifu, sambamba na kuimarisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni kwa wasichana, kwani wao ndio msingi wa malezi na elimu, sambamba na kutumia muda kwa kujifunza mambo yenye manufaa duniani na akhera.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: