Kiongozi wa idara ya taaluma na mitandao Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “App ya Haqibatumu-Umin ambayo ni miongoni mwa App za kiislamu, imezishinda App nyingi za mfano wake, hususan katika misimu ya ibada ukiwemo mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Akaongeza kuwa: “App imepata idadi kubwa ya wanufaika ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, takwimu ziko kama ifuatavyo:
- 1- Zaidi ya mara milioni (30) za usomaji wa Quráni kwa kutumia App ya Haqibatumu-Umin.
- 2- Zaidi ya mara milioni (30) za usomaji wa dua kwa kutumia App ya Haqibatumu-Umin.
Akasema kuwa: “Miongoni mwa huduma muhimu zilizo tolewa na App hiyo katika mwezi wa Ramadhani ni kipengele cha ziara kwa niaba ya maelfu ya waumini kutoka kila sehemu ya dunia, sambamba na kuendesha shindano la wasichana ambalo pia wameshiriki maelfu ya wadau wa App hiyo katika mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.
Akafafanua kuwa: “App hii ni ya kwanza kwa kupakuliwa zaidi hapa Iraq, takwimu zinaonyesha kama ifuatavyo:
- - App imepakuliwa na watu zaidi ya milioni tisa.
- - Inazaidi wa watumiaji hai kila mwezi zaidi ya milioni moja.
- - Kila mwezi kuna watu zaidi ya laki tatu wanao pakua.
- - App imeenea zaidi duniani, inatumika katika nchi zaidi ya (146).
- - Idadi ya swala za faradhi zilizo lipwa kupitia App hiyo zimefika (400,000,000) milioni mia nne.
- - Idadi ya swala za faradhi zilizo lipwa ndani ya mwezi wa Ramadhani ulio isha zimefika milioni (35) kila siku zilikuwa zinalipwa zaidi ya swala milioni moja.
- - App inafanya kazi kwenye zaidi ya aina (190) za simu kutoka mashirika tofauti bila usumbufu wowote, tofauti na App zingine ambazo huchagua aina ya simu”.
Kumbuka kuwa unaweza kupakua App hii kupitia (Google Play)
au kupitia (App Store).