Mwezi nane Shawwal ni siku ya kukumbuka kuvunjwa kwa makaburi ya Baqii

Maoni katika picha
Kila mwaka siku kama ya leo –mwezi nane Shawwal- hurudi upya huzuni za wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa kukumbuka tukio baya lililofanywa na mikono ya madhalimu miongoni mwa maadui zao, kwa kuvunja makaburi ya Maimamu watakatifu (a.s) na kudhalilisha utukufu wao.

Historia inatuhadithia kuwa; ulikuwa ni muendelezo wa chuki za mababu zao, wakawa mfano bora kwa kuiga tabia za babu zao waliokuwa wajinga, madhalimu na waovu, walishambulia mara mbili kwa lengo la kufuta kabisa athari hizo takatifu.

Shambulio la kwanza: lilifanywa mwaka wa (1220h / 1805m), kisha wakati wa utawala wa Othumaniyya waumini wakarudi kujenga upya tena kwa namna nzuri zaidi, wakajenga kubba na misikiti, waumini wakawa wanakwenda kufanya ziara, mmoja wa wazungu alipo tembelea mji wa Madina baada ya kujengwa upya na utawala wa Uthumaniyya alisema kuwa, hakika mji huu unafanana na mji wa Istambul, ni miongoni mwa miji mizuri duniani, hapo ulikuwa ni mwaka wa (1877 – 1878m) kabla ya mji huo mtukufu kushambuliwa kwa mara ya pili.

Shambulio la pili: lilitokea mwaka wa (1344h / 1925m), wale waovu walirudi kushambulia tena mji mtukufu wa Madina kwa mara nyingine, wakavunja alama takatifu za Maimamu watukufu (a.s) na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), baada ya fatwa iliyo tolewa na viongozi wao, Baqii ikavunjwavunjwa na ukawa uwanja ambao hauonyeshi uwepo wa makaburi, hata kama ukigundua uwepo wa kaburi sio rahisi kujua aliyezikwa hapo, bwana mmoja aitwae (Aildunrita) baada ya mawahabi kuushambulia mji wa Madina na kuuwa maelfu ya raia wema anasema kuwa: “Hakika mji umevunjwa na kubba nyeupe zilizo kuwa zinaonyesha makaburi ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) zimesambazwa, na kaburi zingine zote zimevunjwa na kusambazwa”.

Tambua kuwa Baqii kuna idadi kubwa ya kaburi za maswahaba na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) wakiwemo Maimamu wane ambao ni (Imamu Hassan bun Ali Azzakiy, Imamu Ali bun Hussein Sajjaad, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir na Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s).

Hakika Baqii itaendelea kuwa jeraha lisilopona kizazi baada ya kizazi.. na itaendelea kuwa kielelezo cha wazi cha udhalimu wa watawala walio tangulia namna walivyo wafanyia watu waliokuja kuwatoa katika giza na kuwatia katika nuru, walivyo washambulia na kufuta athari zao hadi kupiga marufuku kutembelewa, lakini sisi tunaamini kuwa jeraha la Baqii litakumbukwa daima na hiyo ndio hali inayo shuhudiwa hii leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: