Arshu-Tilawah inaendeleza ratiba yake ya usomaji wa Quráni kupitia matangazo mubashara.

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na ratiba yake ya usomaji wa Quráni kila siku ya Ijumaa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kipindi cha matandazo mubashara.

Kiongozi wa kituo cha habari za Quráni Ustadh Mustafa Daámiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: Usomaji wa Quráni unafanywa kwa kufuata kanuni zote za afya ikiwa ni pamoja na kujiepusha na mikusanyiko ya watu, na kutosheka na kurusha mubashara usomaji huo kwenye kituo cha luninga na watu kufuatilia usomaji huo kupitia kituo cha Karbala wakiwa majumbani kwao au kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Akabainisha kuwa: “Wasomaji wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ambao ni, Sayyid Hussein Halo na Muhammad Ridhwa Salmaan pamoja na Ammaar Hilliy kutoka Atabatu Abbasiyya wameshiriki kwenye vipindi hivyo”.

Akasema: “Miradi mingi ya Quráni tukufu ukiwemo huu wa Arshu-Tilawah, unaolenga kunufaika na vipaji vya wairaq na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kuvilea na kuviendeleza chini ya walimu mahiri, mradi huu unamchango mkubwa, na idadi kubwa ya watu imeshiriki, ulisimama kidogo baada ya kuingia janga la virusi vya Korona na kurudi tena katika sura mpya kulingana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: