Kituo cha taaluma za namba kinafanya nadwa kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Mustanswariyya

Maoni katika picha
Kituo cha taaluma za namba chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya nadwa kwa njia ya mtandao (Webinar) yenye anuani isemayo “Usomaji na utafiti katika mazingira ya janga la Korona”.

Mtoa mada ni Ustadh Ammaar Hussein Jawaad kutoka kituo cha taaluma za namba, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika mada hiyo tumejibu maswali mengi kutoka kwa wahudumu wa maktaba kuhusu mambo wanayo takiwa kufanya wakati huu wa janga la virusi vya Korona duniani, na namna gani maktaba zinaweza kuendelea kuwa na vitabu vya masomo mbalimbali wakati huu wa maambukizi ya virusi vya Korona na tukaitumia maktaba ya Atabatu Abbasiyya kama mfano”.

Washiriki wameonyeshwa kufurahi, na waliendelea kuuliza maswali na kujadiliana baada ya kumaliza muda wa nadwa, aidha wamesifu miradi ya elimu inayo simamiwa na kituo hicho, ukiwemo mradi wa “kulinda matokeo ya elimu hapa Iraq” sambamba na kutaja baadhi ya vipengele vya miradi inayo tekelezwa.

Kumbuka kuwa huduma ya kuazima vitabu kwa njia ya mtandao bado inaendelea, makumi ya wasomi na watafiti wananufaika nayo kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: