Kwa kutumia njia ya mtandao zaidi ya washiriki (40) wamepatikana: Maahadi ya Quráni tukufu inaendesha semina ya naghma za usomaji wa kiiraq

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu –tawi la Najafu- imetoa mafunzo ya naghma za usomaji wa kiiraq na zaidi ya watu (40) wameshiriki kwenye mafunzo hayo kwa kutumia njia za mawasiliano ya kijamii ambayo inamuwezesha mkufunzi kutoa maelekezo kwa mwanafunzi, huku mwanafunzi akipata maelekezo hayo moja kwa moja akiwa nyumbani, wametumia utaratibu huo kutokana na maelekezo ya wizara ya afya baada ya kutokea kwa janga la virusi vya Korona.

Haya yameelezwa na kiongozi wa tawi hilo Sayyid Muhandi Majidi Almiyali, amesema: “Mafunzo ya naghma za usomaji wa kiiraq ni moja ya kozi ambazo hutolewa na tawi hili, kutokana na mazingira ya sasa pamoja na umuhimu wa kuendeleza masomo ya Quráni, tumeamua kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii kufundishia”.

Akabainisha kuwa: “Kozi hii inasimamiwa na msomaji Humaam Swafi Tufaili, ambaye anafundisha namna ya kusoma naghma tofauti za Quráni, pamoja na kufafanua aina za visomo na naghma sahihi zinazo endana na mahadhi ya usomaji wa kiiraq, hii ni kozi muhimu sana kwani inasaidia kutambua na kuinua vipaji vya wasomaji wa kiiraq na kuwatoa mbele katika majukwaa ya usomaji wa Quráni”.

Kumbuka kuwa idara ya Maahadi imechukua hatua madhubuti za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kwa ajili ya kulinda usalama wa afya za watumishi wake pamoja na kuendelea kwa harakati zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: