Idara ya mawakibu za wilaya ya Aziziyyah chini ya mkoa wa Waasit ni miongoni mwa idara ambazo zimetoa misaada kwa familia za wahanga wa marufuku ya kutembea iliyo wekwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, toka siku za kwanza yalipotolewa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, nayo ni sehemu ya program ya kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, bado wanaendelea kutoa misaada kwa kufuata ratiba maalum ya misaada ya kibinaadamu, ndani ya muda mfupi uliopita wamefanikiwa kugawa vifurushi vya nafaka za chakula (24,839), vilivyo kuwa na vyakula vibichi na vilivyo pikwa pamoja na nyama na vinginevyo.
Haya yamesemwa na bwana Samiir Swabriy kiongozi wa idara, akaongeza kuwa: “Wilaya ya Aziziyyah inawatu wenye utamaduni mzuri wa kijamii, mawakibu zetu zinatokana na watu hao, zinawajua watu walioathiriwa na mazingira ya sasa, hivyo zimejitolea kuwasitiri, jambo ambalo limepokelewa vizuri, tumefanikiwa kugawa vifurushi vya chakula cha aina mbalimbali, ambacho tunaamini kinasaidia kupunguza ugumu wa mazingira waliyo nayo kwa sasa, bado tunaendelea kutoa misaada hadi janga hili litakapo isha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.
Akabainisha kuwa: “Kwa mawasiliano zaidi na kuhakikisha tunafikisha chakula kwa kila familia yenye mahitaji, tumeunda kamati inayo tokana na wajumbe wa mawakibu za Husseiniyya pamoja na taasisi za kijamii zilizopo ndani ya wilaya hii, ili ugawaji ufanyike vizuri na kwa uadilifu, katika program hii jumla ya mawakibu (18) zimeshiriki, hawajaishia kugawa chakula peke yake bali wameshiriki pia katika shughuli za kupuliza dawa”.
Kumbuka kuwa program hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu pia ni sehemu ya mkakati wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia wawakilishi wao waliopo mikoani, kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na bado mawakibu Husseiniyya zinaendelea kutoa misaada kwa familia hizo.