Kifaa tiba cha kisasa katika kutibu tatizo la sukari ndani ya hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel inamiliki kifaa tiba cha (Microseen) na (Darumaseen jel) kwa ajili ya matibabu ya majeraha kwa watu wenye maradhi ya sukari, jumla ya wagonjwa elfu kumi kutoka mikoa tofauti ya Iraq wamenufaika.

Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya Alkafeel bwana Ahmadi Ni’mah amesema kuwa: “(Microseen) ni miongoni mwa vifaa vya kisasa katika kutibu maradhi ya sukari, pia ni rahisi kutumiwa na kila mgonjwa na huponyesha haraka”.

Akaongeza kuwa: “Hospitali imeweka kifaa hicho na kutoa maelekezo ya lazima ya namna ya kukitumia, ambapo mgonjwa anaweza kukitumia akiwa nyumbani huku anawasiliana na daktari wake, wakati wa kusafisha jeraha na kutoa nyuzi zilizo haribika, lakini ni muhimu aendelee kuwa chini ya uangalizi wa Daktari, ili kuhakikisha anatumia kwa usahihi”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kila siku inajitahidi kutoa huduma bora kwa vifaa tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa wa kitaifa na kimataifa, jambo ambalo limeifanya kutoa ushindani kwa hospitali kubwa duniani.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari waliobobea katika fani mbalimbali kutoka kila sehemu ya dunia, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote waliopo katika hali zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: