Program ya (mambo ya kifamilia) imeongeza harakati zake

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuongeza harakati zake za (mambo ya kifamilia) kwa njia ya mtandao kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona na tahadhari ya kuepuka misongamano ya watu, harakati hizo zinalenga kujenga utulivu wa nafsi na akili kwa wanafamilia chini ya kauli mbiu isemayo (familia ni amana yangu), tunatoa ushauri nasaha kwa wanafamilia wa rika zote chini ya wataalamu waliobobea katika fani hiyo.

Mkuu wa kituo hicho Ustadhat Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Katika mazingira ya kawaida tumezowea kuwasiliana na wanafamilia pamoja na wasimamizi wa nyumba na watu wa rika zote, aidha huwa tunawapokea katika ofisi zetu na kujibu maswali yao au kutatua shida zao, lakini kutokana na mazingira ya sasa na ulazima wa kuchukua tahadhari za kiafya kwa ajili ya kujikinga na maambuizi ya virusi vya Korona, tumelazimika kutumia jukwaa la mitandao ya mawasiliano ya jamii katika kujibu maswali na kutatua shida za wadau wetu, huduma hii imepata mwitikio mkubwa”.

Akaongeza kuwa: Hivyo tumelazimika kuongeza idadi ya mitandao yetu, pamoja na wataalamu, pia tumeongeza muda wa kupokea maswali na taarifa kupitia mitandao ifuatayo:

  • 1- Mtandao wa mambo ya kinafsi: https://forms.gle/YecoSuigGC9PrbGB7
  • 2- Mtandao wa mambo ya familia na ndoa: https://forms.gle/aXKxPJZDqW8LhXy48
  • 3- Mtandao wa vijana: https://forms.gle/joWUaHWt9dWgvkMa9
  • 4- Mtandao wa watoto: https://forms.gle/GCrUmPZuGgHdkBj47
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: