Kamati ya maandalizi na kamati ya elimu zinazo simamia kongamano la makumbusho ya Alkafeel awamu ya tatu zinajadili uwezekano wa kufanya kongamano hilo kwa njia ya mtandao kutokana na uwepo wa hatari ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi na kamati ya elimu zinazo simamia kongamano la makumbusho ya Alkafeel awamu ya tatu, ambalo liliahirishwa kwa ajili ya kuangalia hali ya maambukizi ya virusi vya Korona, zimefanya mkutano wa kujadili uwezekano wa kufanya kongamano hilo kwa njia ya mtandao kutokana na kuendelea kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona hadi sasa.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim Zaidi amesema kuwa: “Kongamano la makumbusho ya Alkafeel ambalo lilikuwa lifanywe chini ya kauli mbiu isemayo: (Makumbusho na teknolojia za kisasa), ni miongoni mwa makongamano ambayo husimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, awamu mbili zilizo pita zilikua na mafanikio makubwa, kutokana na uwepo wa janga la Korona awamu hii imelazimika kuahirishwa, na sasa tumefanya mkutano huu kujadili uwezekano wa kufanya kongamano hilo kwa njia ya mtandao au tuendelee kusubiri hadi maambuizi ya virusi vya Korona yatakapi isha”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya majadiliano makali tulikuja na nukta nyingi, kubwa ikiwa ni uwezekano wa kufanya kongamano hilo kwa njia ya mtandao, kutokana na kuendelea kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, ukizingatia kuwa mwanzo wa mwaka mpya wa masomo umesha ainishwa”.

Kumbuka kuwa kongamano hulenga mambo yafuatayo:

  • - Kutoa wito wa kulinda turathi na utamaduni.
  • - Kusaidia taasisi za Dini na za kiraia zinazo anzisha makumbusho na kuendeleza utendaji wa makumbusho.
  • - Kufungua milango ya kushirikiana na taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa.
  • - Kuongeza ufanisi katika utendaji wa idara za makumbusho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: