Maahadi ya Quráni tukufu imetangaza mafunzo ya hukumu za usomaji wa Quráni na imetoa wito kwa kila anayependa kushiriki kwenye mafunzo hayo

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia tawi lake la Najafu, imetangaza azma ya kufundisha hukumu za usomaji wa Quráni kwa kutumia mtandao (elimu masafa), siku nne kwa wiki chini ya ukufunzi wa Ustadh Ahmad Zaamiliy.

Kiongozi wa tawi la Maahadi Sayyid Muhanad Majidi Almiyali amesema kuwa: “Tawi letu limezowea kuandaa semina mbalimbali za Quráni katika kipindi chote cha mwaka, lakini kutokana na mazingira ya sasa pamoja na maagizo ya idara ya afya na muongozo wa Marjaa Dini mkuu wa kututaka tujiepushe na mikusanyiko kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, tumelazimika kuendesha semina kwa njia za mitandao, ikiwemo semina hii”.

Akaongeza kuwa: “Semina itafanyika kila siku ya Jumamosi, Jumapili, Jumanne na Ijumaa, kuanzia saa kumi Alasiri, watafundishwa hukumu za usomaji wa Quráni, kuanzia matamshi ya herufi, sifa na hukumu zake”.

Akamaliza kwa kusema: “Hii ni moja ya semina nyingi za ufundishaji wa hukumu za usomaji wa Quráni zinazo fanywa na tawi hili la Maahadi”.

Kumbuka kuwa semina zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni tukufu ni sehemu ya harakati zake muhimu, Maahadi inazipa kipaombele kikubwa kutokana na faida inayopatikana kwenye semina hizo kwa kupatikana kizazi cha wasichana wanaosoma Quráni kwa ufasaha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: